HabariSiasa

WAGOMBEA 6 WA VITI VYA USENETA NA UWAKILISHI WA KIKE KAUNTI YA KWALE WAKOSA KUIDHINISHWA NA TUME YA UCHAGUZI NCHINI IEBC.

Jumla ya wagombea 6 wa viti vya useneta na uwakilishi wa kike kaunti ya Kwale wamekosa kuidhinishwa na tume ya uchaguzi nchini (IEBC) baada ya zoezi hilo kukamilika hapo jana.
Kulingana na meneja wa uchaguzi kaunti hiyo Obadiah Kariuki, wagombea 4 kati ya 13 wa useneta walikosa kuidhinishwa na tume ya IEBC baada ya kukosa kuafikia vigezo hitajika.
Kariuki amedokeza kwamba wagombea hao huru walikosa kufikisha sahihi elfu 2 zinazohitajika huku wengine stakabadhi zao zikikumbwa na dosari.
Wakati huo huo, meneja huyo amesema kuwa wagombea 2 kati ya 8 wa uwakilishi wa kike waliokosa kuidhinishwa, mmoja hakuwasilisha stakabadhi zake kwa IEBC ili zikaguliwe.
Seneta wa Kwale Isaa Boi anayekitetea kiti hicho kupitia chama cha ODM, mgombea wa kiti cha mwakilishi wa kike kupitia chama cha UDA Bibi Masha na mwenzake Zainab Chitsangi ambaye ni mgombea huru wameidhinishwa na IEBC.

>>News Desk.