HabariSiasa

Mgombea wa useneta kaunti ya Kilifi kwa chama cha PAA Ben Kai amepuuzilia mbali kashfa za ufisadi zilizotolewa dhidi yake.

Mgombea wa useneta kaunti ya Kilifi kwa chama cha Pamoja African Alliance-PAA Ben Kai amepuuzilia mbali kashfa za ufisadi zilizotolewa dhidi yake na tume ya maadili na kupambana na ufisadi nchini EACC.
Kulingana na ripoti iliyotolewa na tume ya EACC inaonesha kuwa Kai ni miongoni mwa wagombea wanaohusishwa na kashfa za ufisadi akituhumiwa kuhusika katika ufujaji wa takriban shilingi milioni 250 mnamo mwaka 2015 akiwa katibu katika wizara ya fedha kaunti hii ya Kilifi.
Ripoti hiyo ilitumwa kwa tume ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC ikilenga kuwafungia nje wagombea wanaohusishwa na ufisadi kutojumuishwa kwenye kinyang’anyiro cha nyadhifa za uongozi kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Hata hivyo ametoa wito kwa tume ya EACC pamoja na IEBC kutoa ushahidi wa madai hayo.

>> News Desk…