HabariMombasaNews

Idara ya usalama katika eneo la Likoni yakanusha madai ya maafisa wa polisi kuwahangaisha wahudumu wa Boda boda.

Idara ya usalama katika eneo la Likoni Hapa Mombasa imekanusha madai ya maafisa wa polisi kuwahangaisha wahudumu wa Boda boda katika eneo hilo.

Mkuu wa Polisi eneo hilo Timothy Mwasia amesema maafisa wa Polisi wanatekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria na wala sio kuwahangaisha wahudumu hao.

Mwasia amengeza kuwa maafisa wa polisi vile vile hawahusiki na vitendo vya kuhangaisha wananchi wasio na hatia.

BY EDITORIAL DESK