HabariNewsSiasa

Kwale imepiga hatua kubwa katika uongozi wa akina mama.

Idadi ya wanawake iliyojitokeza kupigania viti vya kisiasa kaunti ya Kwale imetajwa kuongezeka kwa kiwango kikubwa katika uchaguzi uliopita.

Haya ni kwa mujibu wa baraza la kitaifa la makanisa nchini (NCCK) inayosema kuwa idadi hiyo imeongezeka kufuatia hamasa zinazotolewa kwa wanawake kupitia mradi wa Wadada wa Pawa.

Mwenyekiti wa baraza hilo katika eneo la Pwani Askofu Peter Mwero amesema kwamba mradi huo umewapa wanawake motisha ya kuwania nyadhifa za uongozi.

Kwa upande wake mwakilishi wa wanawake katika baraza hilo Eda Wamboi amesema kuwa kaunti ya Kwale imepiga hatua kubwa katika uongozi wa akina mama licha ya jamii kushikilia maswala ya utamaduni na dini dhidi ya wanawake.

BY EDITORIAL DESK