HabariNews

Gavana wa kaunti ya Mombasa Abdhulswamad Nassir amefungua rasmi bunge la 3 la kaunti ya Mombasa hii leo.

Hii ni baada ya kukamilika kwa Mafunzo ya wawakilishi kuhusu namna ya kutekeleza majumu yao yaliyofanyika jijini Nairobi baada ya kuapishwa rasmi.

Nasri amefungua bunge hilo kama gavana wa pili wa kaunti ya Mombasa, na ajenda yake kuu ni kuhakikisha wajumbe hao wanamsaidia kutambua jumla ya watu mia nne wenye uhitaji katika kata zao ili kufaidika na ufadhili wa kaunti.

Wakati wa maadhimisho ya sherehe za mashujaa wiki jana, gavana nassir alisema mia nne hao ni wanafunzi 200 kupata ufadhili wa masomo, na wazee 200 kutoka familia zenye uhitaji ili kufaidika na ufadhili ya malipo ya bima ya afya ya Kitaifa NHIF.

BY EDITORIAL DESK