HabariNews

Idadi ya wanafunzi inayojiunga na shule za upili imetajwa kuongezeka kaunti ya Kwale.

Idadi ya wanafunzi inayojiunga na shule za upili imetajwa kuongezeka kaunti ya Kwale tangu kuanzishwa kwa mpango wa serikali wa kuhakikisha asilimia 100 ya wanafunzi inajiunga na shule hizo.

Kwa mujibu wa naibu kamishna wa Msambweni Kipkoech Lotiatia, idadi hiyo imeongezeka kufuatia ushirikiano wa maafisa wa utawala na washikadau wa elimu katika eneo hilo.

Aidha Lotiatia amesema kuwa tayari watoto wanaojiunga na shule za upili wanazidi kuwa wengi baada ya serikali kuanzisha mpango huo.

Kwa upande wake mwakilishi wa wadi ya Ramisi Hanifa Mwajirani ameitaka idara ya usalama katika eneo hilo kuanzisha kampeni ya kuwasaka watoto wa kike waliosalia nyumbani ili kuhakikisha wanaendelea na masomo yao.

BY EDITORIAL DESK