HabariNews

Wakaazi wa kaunti ya Kwale wamtaka rais William Ruto kurudisha chini bei ya bidhaa za chakula.

Wakaazi wa kaunti ya Kwale wamtaka rais William Ruto kurudisha chini bei ya bidhaa za chakula ili mwananchi wa kawaida aweze kukidhi familia yake ikizingatiwa kwamba baadhi ya sehemu zimeathirika na ukame.

Wakaazi hao wamedokeza kuwa hali hiyo imechangiwa na kupanda kwa bei ya mafuta nchini jambo lililotajwa kumkandamiza mwananchi wa kawaida.

Wakiongozwa na Johnson Okwere amesema kuwa sasa bei vyakula kama unga wa mahindi,maharagwe, sukari zimepanda na ndio chanzo cha kudorora kwa uchumi nchini.

Kwa sasa wakaazi hao wanaiomba serikali kuu kuthamini bei hizo kwa kumfikiria wananchi wa kawaida ambaye maisha yake ni ya chini mno.

BY EDITORIAL DESK