HabariNews

Kenya imetajwa kuwa miongoni mwa mataifa yenye idadi kubwa ya wanafunzi Marekani.

Kenya imetajwa kuwa miongoni mwa taifa lenye idadi kubwa ya wanafunzi wanaosomea taaluma mbalimbali katika taifa la Marekani kutoka barani Afrika.

Haya ni kulingana na mshirikishi wa elimu katika ubalozi wa Marekani Jennifer Maende.

Maende amesema kuwa idadi hii kubwa inasababishwa na taifa la Marekani kuwa na mojawapo ya elimu bora ulimwenguni.

Maende amedokeza kuwa ikizingatiwa kuwa wanafunzi wanaosemea Marekani wanapata fursa ya kupata uzoefu wa kazi imerahisisha wengi wao kuajiriwa katika sekta mbalimbali ulimwenguni.

Anasema shule za Marekani zinatoa ufadhili mzuri wa elimu kwa wanafunzi kutoka kote ulimwenguni.

Maende anasema kivutio kikubwa cha elimu ya marekani ni kusoma na wanafunzi kutoka duniani kote na kusoma tamaduni tofauti za ulimwengu.

BY EDITORIAL DESK