HabariNews

Jamii ya wakaazi wa kwale yashauriwa kutafuta suluhu ya matatizo yao badala ya kujitoa uhai.

Kitengo cha usalama eneo bunge la Shimba Hills kaunti ya Kwale kinawashauri kina mama na hata jamii kwa ujumla kutafuta suluhu ya matatizo yao badala ya kujitoa uhai.

Hii ni baada ya kubainika kwa kujinyonga kwa mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 26 kutoka kijiji cha Mtsangatamu wadi ya Mkongani.

Kulingana na Afisaa wa usalama kutoka eneo bunge hilo Elizabeth Ngumbau, amethibitisha tukio hilo huku akisema tayari uchunguzi unaendelea kwani mama huyo amepatikana akining’inia kwenye mkorosho karibu na nyumba yake.

Kulingana na Ngumbau mama huyo aliyewaacha watoto wanne nyuma, kifo chake kimetajwa kuhusishwa na mzozo wa kimapenzi.

BY EDITORIAL DESK