HabariNews

Shirika la kitaifa la kutetea haki za kibinadamu la (KNCHR) limesema kuwa linalenga kukabiliana na visa vya dhulma za kijinsia.

Shirika la kitaifa la kutetea haki za kibinadamu la (KNCHR) limesema kuwa linalenga kushirikiana na mashirika ya kijamii ili kukabiliana na visa vya dhulma za kijinsia.

Mwenyekiti wa shirika hilo Roseline Odede ameahidi kushirikiana na shirika la HURIA ili kukomesha visa hivyo vilivyokithiri katika kaunti ya Kwale.

Akizungumza katika eneo la Kinango, Odede amesema kuwa afisi hiyo itawasaidia waathiriwa kupata haki yao.

Kwa upande wake mkurugenzi wa shirika hilo Yusuf Lule amesema kuwa visa vya dhulma, mizozo ya ardhi na mauaji ya wazee vimekithiri katika eneo hilo.

Hata hivyo, Lule amedokeza kwamba tayari kesi 18 zimetatuliwa na shirika hilo tangu kufunguliwa kwa afisi hiyo.

BY EDITORIAL TEAM.