HabariNews

Wazazi Kaunti ya kwale watakiwa kuchukua tahadhari dhidi ya watoto wao kurandaranda katika fuo za bahari.

Naibu kamishna eneo la Msambweni kaunti ya Kwale Lotiatia Kipkech amewataka wazazi kuchukua tahadhari ya watoto wao dhidi ya kurandaranda ovyo katika fuo za bahari msimu huu wa sherehe za krismas kuwa hatua hio huenda ikahujumu usalama wao.

Lotiatia anasema kwamba eneo la Diani na Ukunda kwa sasa inashuhudia idadi kubwa ya wageni mbalimbali akihofia kuwa huenda wahalifu wakatumia msimu huu kuendeleza biashara za usafirishaji watoto ama kuwashawishi kujiingiza katika vitendo haramu.

Amewataka wakaazi kuripoti visa vyovyote vinavyolenga kuhujumu usalama katika eneo hilo.

BY EDITORIAL TEAM.