HabariNews

Onyo kali latolewa kwa maafisa wa umma hususan wale wa idara ya afya wanaozembea kazini.

Onyo kali latolewa kwa maafisa wa umma hususan wale wa idara ya afya wanaozembea kazini mwao kuwa hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yao.

Haya ni kwa mujib wa gavana wa Kwale Fatuma Achani alipotangaza mabadiliko katika usimamizi wa hospitali ya Mjini Kwale huku akiwataka maafisa hao kuwajibika ili kuhakikisha kwamba hakuna huduma zozote zitakazolemazwa.

Aidha Achani ameendelea kusema kuwa Serikali ya Kaunti ya Kwale imeipa kipaumbele sekta ya afya, hivyo basi hatarajii kamwe kuwe na lalama kutoka kwa wananchi kuhusu ukosefu wa huduma bora katika vituo vya afya na zahanati za kaunti hiyo.

BY EDITORIAL DESK