HabariNews

Familia moja katika eneo la Tsimba , Matuga kaunti ya Kwale kupokea mwili wa mpendwa wao.

Familia moja katika eneo la Tsimba , Matuga kaunti ya Kwale kupokea mwili wa mpendwa wao hivi leo siku ya Jumatano kutoka nchi ya Qatar ambapo msichana huyo alikuwa akifanya kazi ya nyumbani.

Bintimohammed Ali Mwanyota alifariki mnamo tarehe 4 mwezi huu baada ya kuweka jiko la makaa katika chumba alichokuwa akilala kutokana na baridi .

Akiwa mwingi wa huzuni Hamisi Omar Mwanyota ambaye ni baba mdogo wa mwendazake mwenye umri wa miaka 32 anasema kuwa walipata habari ya kifo cha mwanawe baada ya kupigiwa simu na tajiri wake kutoka nchini Qatar.

 

Marehemu ameifanyia kazi familia hiyo kwa zaidi ya miaka 6 na mara ya mwisho kuwa humu nchini ilikuwa mwezi Machi mwaka uliopita 2022 alipokuja mapumzikoni.
Athman Salim Mwatesfu ni kaka wa marehemu na anasema kuwa matayarisho ya mazishi yanaendelea wakitarajia kupokeea mwili huo hivi leo

 

Faida Amboe ni mkoi wa marehemu na anasema kuwa marehemu amewacha watoto wanne wa kike mkubwa akiwa kidato cha pili na mdogo akiwa na umri wa miaka 4.
Aidha familia ya tajiri wake nchini Qatar imesimamia kusafirisha mwili huo hadi hapa nchini.

BY EDITORIAL DESK