HabariNews

Tatizo la uhaba wa ajira  humu nchini linawapelekea wakenya wengi kutafuta kazi ughaibuni ili waweze kukidhi mahitaji yao.

Tatizo la uhaba wa ajira  humu nchini linawapelekea wakenya wengi kutafuta kazi ughaibuni ili waweze kukidhi mahitaji yao.

Haya ni kulingana na Hamisi Mwanyota mkaazi wa eneo la Tsimba Kaunti ya Kwale ambaye anasema kuwa watu wanaoelekea nchini za Uarabuni kutafuta ajira hawafai kulaumiwa kwani wanajitafutia riziki.

Mwanyota anasema kuwa mshahara unaolipwa ughaibuni hata kwa mfanyikazi wa nyumbani ni kiwango cha juu kuliko hapa nchini.

Mkaazi huyo ameitaka serikali kuweka mikakati ili nafasi za ajira zipatikene hapa nchini na kukomesha wananchi kusafiri hadi ughaibuni kusaka ajira.

BY EDITORIAL DESK