HabariMombasa

Halmashauri ya Bandari KPA yatoa Msaada wa chakula eneo la Kinango kaunti ya Kwale.

Halmashauri ya Bandari nchini KPA imetoa msaada wa chakula chenye thamani ya shilingi milioni 1.5 kwa familia zilizoathrika na ukame eneo la Kinango kaunti ya Kwale.

Msaada huo uliotolewa na mwenyekiti wa bodi wa Bandari nchini Benjamin Tayari,umefaidi zaidi ya familia elfu 1 kutoka meneo ya Ndavaya na Lustangani ,maeneo yaliyoathirika zaidi na ukame eneo hilo.

Mwenyekiti huyo amedokeza kuwa Halmashauri hiyo itajihadi kusaidia iwezapo kwa wakaazi ambao wameathirika zaidi na baa la njani msimu huu wa ukame.

Amesema kuwa wanafanya kazi kwa karibu na serikali ya kaunti ya Kwale kusaidia juhudi za wasamaria wema, waliona malengo kupunguza makali ya njaa kaunti ya Kwale.

Kwa upande wake naibu kaunti kamishna wa kinango Abdullahi Galgalo, ameishukuru uongozi wa Bandari kwa kusaidia zaidi ya watu elfu 38 ambao wanapitia hali ngumu katika eneo hilo.

Miongoni wa waliohudhuria zoezi hilo la ugavi wa chakula ni akiwemo ni meneja wa mawasiliano wa kpa Benard Osero na mwakilishi wadi wa Ndavaya Ali Beja.

Kulingana na kamati ya kushughulikia janga la Ukame kaunti ya Kwale , zaidi ya watu laki 2 eneo la Kinango, Shimba Hills, Samburu na Lunga Lunga wanauhitaji mkubwa wa chakula na maji wakati huu.