HabariNews

MAANDAMANO YATAENDELEA KILIFI ASISTIZA SPIKA WA BUNGE LA KILIFI.

Spika wa bunge la kaunti ya KIlifi Teddy Mwambire aliyepa mwenyekiti wa chama cha ODM kaunti ya Kilifi amesistiza kuwa maandamano yataendelea kama yalivyopangwa kaunti hiyo.

Muungano wa Azimio la Umoja One Kenya umesistiza kuwa maandamano yaliyopangwa kufanyika Jumatano wiki hii yataendelea licha ya onyo kali kutoka kwa waziri wa usalama Kithure Kindiki.
 
Kulingana na spika wa bunge la kaunti ya Kilifi Teddy Mwambire, Onyo iliyotolewa na Kindiki haina mshiko wa kikatiba, jambo analosistiza kuwa linawapatia uhuru wa kuendelea na maandamano hayo.Aidha ameeleza kuwa maandamano hayo yataendelea mpaka pale serikali itakapo kubali kutafuta suluhu ya hoja zilizotolewa na wananchi. Miongoni mwa hoja hizo ni gharama ya juu ya maisha.

BY ERICKSON KADZEHA