HabariLifestyle

Serikali kuharakisha mchakato wa utoaji leseni kwa Base Titanium Kaunti ya Kwale.

Serikali ya kitaifa kupitia Wizara ya Madini na Leba imebaini kuharakisha zoezi la utoaji wa leseni ili kuhakikisha kuwa kampuni hiyo inaendeleza shughuli zake.

Waziri wa Leba Florence Bore aliyekuwa akizungumza baada ya kuzuru kampuni hiyo amefichua kuwa tayari taratibu za utoaji wa leseni zinakaribia kukamilika huku akisema kuwa amefanya mazungumzo na waziri wa madini Salim mvurya ili kufanikisha zoezi hilo.

“Nataka tu niwahakikishie kuwa kampuni (Base Titanium) haitafungwa, na kwamba serikali ilikuwa imetoa ile kitu inaitwa monitorial. Kwamba mining sites kwa nchi zilikuwa zimesimamishwa.” Akasema Waziri.

Bore amesema kuwa kampuni hiyo imeorodhesha bora nchini kutokana na utendakazi wake.

Kwa upande wao viongozi wakiongozwa na Mwakilishi wadi ya Ramisi, Hanifa Mwajirani na mwenzake wa wadi ya Kinondo Juma Maone wameelezea wasiwasi wao endapo kampuni hiyo italazimika kufunga virago vyake mwaka ujao.

Kuna vijana wetu wengi ambao wameajiriwa hap ana wengine wanapata lishe kupitia hapa, hivyo kampuni ikifungwa tunajiuliza watakwenda wapi mwaka ujao.”

Nao wakaazi wa eneo hilo wameomba kuiongezea muda kampuni hiyo wakisema kuwa wakaazi wengi na vijana wamekuwa wakifaidika pakubwa na nafasi za ajira hatua ambayo imetajwa kupunguza visa vya uhalifu kwa kiwango kikubwa.

“Base Titanium ikajaribu kuondoka katika hili eneo hakika akina mama watahangaika, hatujui tutakakoenda.”

Wakaazi wamesisitiza kuwa iwapo kampuni hiyo itafungwa basi visa vya utovu vya usalama huenda vikachipuka tena katika maeneo hayo.