HabariMazingiraNews

Wakaazi wa Kaunti ya Kilifi wahimizwa kupanda miti ili kukabiliana na mabadiliko ya hali anga.

Kaunti ya Kilifi Yawahimiza Wakaazi wa Kaloleni Kupanda Miti kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi

Gavana wa kaunti ya Kilifi Gideon Mung’aro amehimiza wakaazi wa Mwanamwiga eneobunge la Kaloleni kupanda miti kwa wingi hasa msimu huu ambapo mvua kiasi inashuhudiwa.

Aidha Mung’aro amedokeza kuwa serikali ya kaunti hiyo inalenga kupanda miti milioni 10 huku akisema jambo hilo litafanikishwa iwapo wakaazi watakauwa na ushirikiano.

“Tutaanzisha rasmi kupanda miti halafu tutakuwa na mipango maalum kupitia kamati yetu ya Mazingira ili tuhakikishe kuwa tunaboresha hali hiyo. Kama kaunti tuna lengo la kupanda miti milioni 10.” Akasema Mung’aro.

Mung’aro amesisitiza haja ya jambo hilo kushughulikiwa ili kupambana na madadiliko ya tabia ya nchi.

Kwa upande wake chifu wa eneo la Mwanamwiga Joseph Kitsao amehimiza wenyeji kujitolea kwa uhifadhi na upandaji wa miti ili kuzuia mmomonyoko wa udongo.

Natoa wito kwa wakaazi wa Mwanamwinga, Kaloleni, jamani tupande miti kwa wingi kuimarisha mazingira yetu haya tuepuke hizi shida tunazipitia sasa.” Akasema Bw. Chifu.