HabariLifestyleNews

Mahakama Yabuni mbinu ya kuharakisha Kesi mahakamani, Malindi

Mahakama ya Malindi imebuni mfumo mpya wa kuharakisha na kusikilizwa kwa kesi mahakamani.

Mkuu wa mashtaka ya umma katika kaunti ya Kilifi Vivian Kambaga amesema kuwa Mahakama ya Malindi imebuni mfumo mpya wa kuharakisha na kusikilizwa kwa kesi mahakamani.

Kulingana na Vivian mfumo huo ni kama njia mojawapo ya kupunguza mrundiko wa kesi kortini kuokoa muda zaidi, na kumlazimu mshtakiwa kukubali mashtaka yake kwa haraka ili kupunguza kifungu chake.

Aidha amesema kuwa zaidi ya washukiwa 10 kwa sasa wamekubali makosa yao.

“Ni makubaliano baina ya mwendesha mashtaka na mshatakiwa ya kuwa mimi ni kweli nilitenda kile kitendo nitakubali mashtaka lakini mwisho wa siku uamuzi unaotolewa na mwendesha mashtaka hauko sawa na makosa ya mshtakiwa.” Alisema Vivian kambaga

Naibu mkurugenzi mkuu wa kitengo cha urekebishaji tabia Konrad Masinde amesema kuwa mfumo huo umezingatia njia mbali mbali za kusuluhisha kesi mashinani.

Hata hivyo Masinde amebainisha kwamba idara hiyo imetoa ripoti kwa Mahakama kuwafahamisha kuhusu kesi  zinazolengwa kusuluhishwa mashinani.

“kesi nyingi zimefanyika katika familia za kaunti ya kilifi na kuna vitu zinazingatiwa kama njia mbadala ya kutafuta haki wengine wanafanya maslahi na kusuluhisha kwa fidia.” Alisema Naibu Mkurugenzi.