HabariNews

Wakazi ziwa la Ng’ombe Mombasa walalamikia usalama

Wakaazi wa wadi ya ziwa la Ng’ombe eneo bunge la Kisauni hapa Mombasa wametaja Ukosefu wa mataa ya bararani-Mulika Mwizi kuwa  chanzo ta ongezeko la visa vya utovu wa usalama eneo bunge hilo.

Wakiongozwa na Maxwel Khonde aliyegombea wadhifa wa uwakilishi wadi eneo hilo, wamelilamikia ongezeko la visa vya uhalifu hasa nyakati za usiku wakaazi wanaporejea majumbani mwao..

Khonde alishinikiza kuwa anataka viongozi waliomamlakani kuingilia kati ili kuhakikisha wanaweka mataa kama njia ya kudumisha amani wakisema jambo hilo limewakosesha amani kwa muda mrefu.

Wenyeji hao walizua maswali mengi ni kwa nini eneo lao inakosa mataa ilihali maeneo mengine yapo na mataa na usalama umeimarishwa.

Aidha walidai kutengwa katika kupata huduma muhimu na serikali ya kaunti ya Mombasa.

BY EDITORIAL DESK