Uncategorized

Mawaziri Wawajibishwa Mung’aro Akiwakazia kamba Kilifi

Mawaziri wote wa idara za kaunti ya Kilifi leo wametia sahihi mikataba mipya ya utendakazi inayolenga kuhakikisha uwajibikaji bora miongoni mwao.
Shughuli hiyo iliyofanyika katika ofisi ya makaazi ya gavana wa Kilifi Gideon Mung’aro, ni ya kwanza kuwahi kufanyika katika kaunti ya Kilifi.

hatua hio ya kihistoria kulingana na Mung’ro  inalenga kutoa huduma kwa wakaazi wa Kilifi kwa njia bora zaidi.

Haya yanajiri siku chache tu baada ya maafisa 11 wa serikali ya kaunti hio kusimamishwa kazi kwa madai ya ukiukaji wa sheria za utendakazi.

Hata hivyo gavana huyo alito wito kwa mawaziri wasioweza kufanya kazi kuambatana na mikataba hiyo na kujihuzulu, ili kuonyesha mfano bora kwa wakaazi wa kaunti ya Kilifi.

BY EDITORIAL DESK