HabariMazingiraNews

Hali Hatari ya Anga, Chikungunya na homa la Dengue Kusambaa Nchini

Wanasayansi wameitisha ushirikiano Zaidi kwa washikadau kutoka sekta mbali mbali nchini kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na athari zake kiafya.

Wataalamu katika sekta ya afya na Mazingira walibaini kuwa ongezeko la joto limechangia pakubwa matatizo ya kiafya na mkurupuko wa magonjwa nchini na duniani kwa jumla jambo linalo hitaji jitihada za pamoja kukabili changamoto hizi.

Katika kongamano la pili kujadili afya na hali ya anga, Mkurugenzi wa taasisi ya utafiti wa dawa nchini (KEMRI) Elijah Sangok alidokeza kuwa  utafiti ulionyesha  kuwa mabaddiliko ya tabia nchi yanaleta Athari kubwa kwa afya ya  umma.

Ni muhimu kuangazia mafungamano baina ya afya na tabianchi. Ni dhahiri kwamba tumefikia hatua ambayokwamba mafungamano haya hayawezi kudharauliwa au kupuuziliwa” alisema Sangok

Kulingana na mkurugenzi wa shirika la kutoa Mipango ya dawa kwa magonjwa yaliyopuuziliwa (Drugs for Negleted Deseases Initiative) kanda ya Afrika Mashariki Prof. Sam Kariuki, kumeshuhudiwa ongezeko la magonjwa ya kuambukiza kutokana na mabadiliko ya hali ya anga na kuhatarisha Maisha watu.

Prof. Sam alitolea mfano homa ya dengue na virusi vya chikungunya vilivyo tambulika hasa sehemu ya mwambao ambavyo vinaenea sehemu za bara ya nchi .

Ongezeko la joto ulimwenguni linachangia pakubwa ongezeko la mbu na makaazi yake” alisema Kariuki.

Kumeshuhudiwa ongezeko la maradhi kutokana na mabadiliko ya hali ya anga ikiwemo ugonjwa wa Malale, Magonjwa yanayosababishwa na wanyama, magonjwa ya kupumua pamoja na Cancer.

Wanasayansi aidha walitaja ongezeko hili kuwa tatizo kubwa katika utimizaji wa maendeleo Endelevu Nchini.

BY EDITORIAL DESK