HabariNewsSiasa

Fahamu Magavana 21 wanaochunguzwa na EACC kuhusu Ufisadi

Tume ya Maadili na Kupambana na ufisadi nchini (EACC) imeanzisha uchunguzi dhidi ya magavana 21 wanaoandamwa na kashfa mbalimbali za ufisadi.

Magavana hao wanahusishwa na Sakata za ubadhirifu na ufujaji wa mali ya umma, utoaji wa kandarasi haramu, malipo kwa wafanyakazi hewa, miswada haramu na pia uvunjaji wa sheria katika matumizi ya fedha.

Msemaji wa EACC, Eric Ngumbi amekariri kuwa Tume hiyo inawachunguza magavana walioko mamlakani sasa na pia wale ambao hawako uongozini.

Ngumbi ameongeza kwamba uchunguzi dhidi yao unaendelea na watamkabidhi Kiongozi wa Mashtaka ya Umma majina yao pindi tu uchunguzi utakapomilika.

Hata hivyo Ngumbi amepuuzilia mbali madai ya Muungano wa Azimio kwamba vita dhidi ya ufisadi vinalenga mrengo mmoja wa siasa na kuwataka viongozi wa kisiasa kukoma kuingiza siasa katika vita dhidi ya ufisadi.

Spear of Integrity.

Tayari aliyekuwa gavana wa kaunti ya Kakamega Wycliffe Oparanya pamoja na wakeze watatu walihojiwa na Tume ya EACC baada ya operesheni kali kufanyika nyumbani kwao.

Oparanya na familia yake anadaiwa kufuja shilingi bilioni 1.3 za kaunti ya Kkakamega alipokuwa gavana wa kaunti hiyo.

Itakumbukwa kuwa katika Ripoti ya robo mwaka ya EACC iliyochapishwa katika Gazeti rasmi la Serikali mnamo Agosti 11, Tume hiyo ilisema kuwa imewasilisha mafaili kwa Mkurugenzi wa mashtaka ya Umma, DPP ikitaka kushtakiwa kwa Gavana wa Kakamega Farnandes Barasa na aliyekuwa Gavana wa Kitui Bi. Charity Ngilu kwa tuhuma za ufisadi.