HabariMazingiraNews

WAKAZI Kilifi wamekosa Ufahamu kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi

Wakazi wengi kaunti ya Kilifi hawana ufahamu wa kutosha kuhusu maswala ya tabia nchi. Haya yamebainika baada ya kukamilika kwa warsha iliyowaleta pamoja wadau, wanaharakati na mashirika ya jamii yanayojihusishwa na maswala ya tabia nchi mjini Kilifi.
Athari za mabadiliko ya tabia nchi zikiendelea kushuhudiwa kote ulimwenguni, jitihada za kukabiliana na athari hizo zinaendelea kufanywa kwa njia tofauti tofauti.

Kwa sasa, imebainika kuwa wakazi wengi kaunti ya Kilifi hawana ufahamu wa kutosha kuhusu swala la tabia nchi, hili lilibainika wakati wa warsha iliyowaleta pamoja wadau mbali mbali kujadili maswala ya tabia nchi mjini Kilifi Agosti 31, 2023.

Huwenda sehemu mbali mbali katika ukanda wa Pwani zimeathirika na mabadiliko ya tabia nchi ikiwemo maradhi ya kuambukiza. Hii ilidhihirika katika kongamano la afya na mabadiliko ya tabia nchi liliotamatika Agosti 30, 2023.

Kulingana na Bob Aston ofisa wa shirika la Arid Lands Information Network- (ALIN) kwa ushirikiano na East Africa Centre for Human Rights- (EACHRIGHTS) wadau wengi hawafahamu sheria na mikakati ambayo imewekwa na serikali ya kaunti ya Kilifi inayoambatana na maswala ya tabia nchi.

washikadau wengi bado hawajui kuhusu amendment act iliyopitishwa na pia the Kilifi climate change action plan, naleo imetupatia fursa kwanza watu waweze kujua kwasababu around may kaunti ilifanya assessment kuangalia harzards kwa ward level,” alisema.

Bob aliongezea kusema kuwa, hamasa zaidi zitaendelea kutolewa kwa wadau ili kuzidisha ufahamu wao pamoja na kusaidia kupeleka hamasa hiyo mashinani.

Warsha hiyo aidha, inatarajiwa kuwezesha wadau wengi kuanzisha miradi mbali mbali inayolenga kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.

So tunatarajia kupitia hii watu wengi wanaweza kujua kwnza miradi tofauti ya climate change na pia kuhusu mambo ya policy iliwaweze kujua policy ambayo kaunti imeanzisha ama miradi tofauti ya climate change ambayo kaunti inataka kutekeleza na pia kuhusu program ya financing locally led payment action kwasababu hio program ni muhimu sana kwa kaunti, kwasababu miradi tofauti itakuwa ikitekelezwa na ward climate change climate committee” Aliongezea.

Ikumbukwe kuwa Kenya inatarajiwa kuandaa kongamano kuhusu tabia nchi hapa barani Afrika mapema mwezi Septemba.

BY ERICKSON KADZEHA