HabariNews

Mombasa Yajitayarisha Kukabili Mvua za Elnino

Serikali ya kaunti ya Mombasa imebaini kuweka mikakati kabambe ya kukabiliana na mvua za El-nino izilizotabiriwa kuanza kunya mwezi Oktoba.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa Kituo cha Uvumbuzi wa Kijamii, Gavana wa kaunti hiyo Abdulswamad Sharrif Nassir alisema kuwa  mipango ipo tayari kusafisha mitaro na kukarabati mabomba ya majitaka na miundombinu katika baadhi ya maeneo ambayo yamo hatarini kwa mafuriko.

Gavana Nassir alitaja baadhi ya maeneo yalioanza kukarabatiwa ikiwemo Utange, Bomu, Likoni, miongoni mwa maeneo mengine ya kaunti hiyo huku akiahiidi kushirikiana na washikadau mbali mbali ili kujiweka tayari na mvua hizo.

”Tuko tayari ukiangalia sasa tumeanza kusafisha mabomba ili kuzuia mafuriko wakati wa mvua hizi,tunavyoongea maeneo kama vile Utange ,Bomu Likoni miongoni mwa maeneo mengine yanashughulikiwa.”Alisema Nassir

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa shirika la Msalaba mwekundu Dkt. Ahmed Idris alipongeza juhudi za serikali ya kaunti kwa kuendelea kusafisha Mabomba ya maji taka ili kujiweka tayari kwa mvua hio.

“Tuko na furaha kushirikiana na kaunti ya Mombasa kwa kujitayarisha vilivyo katika kusafisha mabomba yam aji na kutoa taka hiyo ni hatua moja na nzuri kuonyesha kuwa tuko tayari na katika serikali ya kitaifa pia shughuli sawia na hiyo inaendelea kwa ushirikiana na wadau mbali mbali.”Alisema Idris .

Haya yanajiri baada Idara ya hali ya Anga kutangaza uwezekano wa kushuhudiwa kwa mvua za Elnino kuanzia mwishoni mwa mwezi Septemba na kuendelea kuwa nyingi zaidi kufikia mwezi Oktoba mwaka huu.

BY EDITORIAL DESK