HabariNews

Ufunguzi wa ‘I.O.Me 001’ Waleta Matumaini ya Ajira Mombasa

Vijana kaunti ya Mombasa na Pwani kwa jumla sasa wana kila sababu ya kutabasamu kufuatia uzinduzi wa kituo cha Uvumbuzi wa Kijamii kitakachowapa fursa ya ajira.

Kituo hicho kwa jina I.O.Me 001 kilichozinduliwa na Shirika la Msalaba Mwekundu kwa ushirikiano na Ubalozi wa Ufaransa nchini na mashirika mengine, kitatoa fursa kwa vijana wenye ujuzi kujiendeleza na kukuza talanta na kutumia ubunifu wao vyema.

Akiongea katika hafla hiyo Balozi wa Ufaransa  hapa nchini na Somali, Arnaud Suquet alibaini kuwa lengo la mradi huo ni kuwapa vijana ujuzi na nafasi mwafaka za kujibunia ajira, huku akiahidi kuunga mkono jamii hiyo ya vijana kimaendeleo.

“Kituo hiki ni kutoa ujuzi na kutengeneza nafasi za kazi kw vijana kwa maana kuwekeza kwa vijana ni kama kuwekesha kwa maisha ya badae na tuna imani kwamba huu mfumo enedelevu kwa vijana.”Alisema Sequet.

Akipongeza ushirikiano huo, Gavana wa Mombasa Abdulswamad Sharrif Nassir aliwataka wawekezaji zaidi kujitokeza kuwekeza miradi yenye manufaa kwa vijana na wakazi wa kaunti hiyo kimaendeleo.

“Nifuraha yangu kuwakaribisha Mombasa Balozi Sequet najua ni na jimbo unaoupenda na ni mji  mtulivu.”Alisema Nassir

BY EDITORIAL DESK