HabariNews

Kampuni Binafsi Zatabasamu KPA ikitaka kubinafsisha baadhi ya ‘GETI’ za Bandari Lamu na Mombasa

KAMPUNI za kibinafsi huwenda zifaidika na mabilioni ya pesa za usimamizi wa bandari nchini, baada ya serikali ya kitaifa kutangaza azma ya kubinafsisha baadhi ya gati kwenye bandari ya Mombasa na Lamu.

Kutokana na tangazo Jumatatu Septemba 11, 2023, Mamlaka ya Kusimamia Bandari za Kenya (KPA) ilionyesha nia kushirikiana na kampuni za kibinafsi kuendesha gati tatu za bandari ya Lamu, nne Mombasa na sehemu maalumu ya zamani ya kuwekea makasha.

Mkurugenzi Mkuu wa KPA, Bw William Ruto, aliomba kampuni kutuma maombi yao kabla Oktoba 12 ili kuorodheshwa kwa kampuni zitakazomiliki sehemu hizo.

KPA inaomba kampuni zilizohitimu kutuma maombi kabla Oktoba 12 mwaka huu ili kupewa fursa ya kusimamia gati (1-4) katika bandari ya Mombasa na bandari mpya ya Lamu yenye gati tatu,” alisema Ruto.

Hata hivyo, mwenyekiti wa Chama cha Kimataifa cha Wasafirishaji na Wenye Mabohari (KIFWA), Roy Mwanthi, aliunga mkono kampuni ya kibinafsi kuendesha bandari ya Lamu.

Kwa upande mwingine mwenyekiti wa Chama cha Kimataifa cha Wasafirishaji na Wenye Mabohari (KIFWA), Roy Mwanthi, aliunga mkono kampuni ya kibinafsi kuendesha bandari ya Lamu.

Bandari ya Lamu inahitaji hilo ili kuiboresha kwani tangu ifunguliwe rasmi mwaka 2021 ni meli 22 pekee zimetia nanga. Hatuna budi kuhusisha kampuni za kibinafsi ilimradi hatua italeta mapato zaidi,” alisisitiza  Mwanthi.

Ikumbukwe kuwa hapo awali, viongozi wa kisiasa eneo la Pwani walikuwa wakipinga kubinafsishwa kwa bandari nchini wakisema kuwa, haitawezekani serikali itumie mabilioni ya fedha kujenga miundomsingi katika bandari kisha ipokeze shirika la kibinafsi kuisimamia.

Hili halikukinzana na baadhi ya viongozi wa mrengo wa Kenya Kwanza kupinga pendekezo la serikali ya Rais mstaafu Uhuru Kenyatta kubinafsisha usimamizi wa bandari ya Mombasa.

Hata hivyo baadhi ya kampuni zilizokuwa zikimezea mate fursa hii huwenda zikatabasamu kutokana na faida kuu itakayotokana na mpango huo.

BY EDITORIAL DESK