HabariNews

Mwili wa Mwanamume wakutwa Ukielea Baharini Oldport Mombasa

Idara ya usalama Mombasa inaendelea na uchunguzi baada ya mwili wa mwanamme mmoja kupatikana ukielea katika ufuo wa Bahari hindi mjini Mombasa.

Afisa wa maswala ya dharura katika shirika la Haki Africa Mathius Shipeta alisema kuwa mwili huo ulitambuliwa na wavuvi eneo la Old port eneo bunge la Mvita nyakati za asubuhi.

Kulingana na Shipeta, huenda marehemu alisombwa na mawimbi ya maji kutoka sehemu nyingine hadi eneo hilo kwani wavuvi walishindwa kumtambua

Mwili wa mwanamume huyo hata hivyo ulipelekwa katika hifadhi ya maiti katika hospitali kuu ya rufaa eneo la pwani maarufu Coast General.

BY EDITORIAL DESK