HabariNews

Jamaa Ashambuliwa na Kujeruhiwa na Nyati, Lamu

Mwanamume mmoja anauguza majeraha mabaya baada ya kushambuliwa na nyati katika kaunti ya Lamu.

Kulingana na Chifu wa eneo la Mpungani Mutakina Hussein, Aboud Hajj mwenye umri wa miaka 27 inadaiwa, alivamiwa na Nyati njiani alipotoka kazini eneo la Kizingo akielekea katika makaazi yake huku wenzake wakifanikiwa kutorokea msituni  katika tukio hilo lililotokea kisiwani Amu.

“ Alikuwa pamoja na wenzake. Walikuwa wametoka Kizingo kuelekea Kipungani tukio hilo lilipotokea,” Hussein alisema

Wakati huo huoWenyeji walimshambulia nyati huyo kwa silaha ghafi na kumuua papo hapo. Majeruhi alikimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya King Fahad kwa ajili ya matibabu.

Shambulizi hili linaongeza idadi ya visa vya wanyama pori kushambulia wakaazi vilivyoripotisa sehemu mbali mbali nchni Kenya. Hili linatia hofu ya kundelea kwa mgogoro baina ya watu na wanyama pori.

kilio na vidole vya lawama vikielekezewa hifadhi za wanyama na shirika la uhifadi wa wanyama hao KWS.

BY EDITORIAL DESK.