HabariNews

Maadhimishi ya wiki kwa Watu wasiosikia Ulimwenguni

Huku ulimwengu ukiadhimisha wiki ya walemavu wa kusikia Septemba 2023, wadau wa elimu ya malumu wametoa wito kwa serikali kuhakikisha walemavu hao wamepata elimu ya kuwsaidia kupata ajira.

Katika ufungu wa maadhimisha ya watu walio na ulemavu wa kusikia katika taasisi ya masomo maalum mjini Nairobi, wazazi walio na watoto walemavu walihimizwa kutowatenga kadhalika wakitakiwa kuwapeleka shuleni kwani yapo masomo yanayowafaa kutambua talanta zao na kujikimu maishani sawia na watu wengine wasio na ulemavu.

Akiongea kupitia lugha ya ishara kwenye  hafla hio, Kamishna katika afisi ya Ombudsman Washington Sati aliitaka viongozi katika serikali kutoa maamuzi yatakayo wasaidia na kutetea haki za watu na jamii wasio sikia nchini.

“Tunajadiliana na wakuu wa maamuzi nchini ndani na nje ya serikali , na tunafuraha kuwa na Bi. Charlene miongoni mwa jamii ya wasio sikia na tumemkaribisha katika jamii yetu ili atusaidie na kutetea haki zetu” Alisema Sati

Kwa upande wake Charlene Ruto alitilia pondo azma ya kushikwa mkono kwa jamii hii katika masuala mbali mbali ikiwemo elimu na kuwapa ujuzi  utakaowanufaisha katika maisha ya mbeleni.

“ tunafaa kusaidia hii jamii ili waweze kufaidika na kunufaika maishani sio tu kwa watu binafsi bali kwa jamii kwa ujumla , kwahio nataka kuwasaidia kielimu, kupata ujuzi ili kupata ajira na ujasiriamali na pia kuwaunga mkono kama jamii tuweze kujifungamanisha pamoja nao.” Aliongezea Charlene

Mada kuu ya wiki hii ikilenga watu wasio sikia kila mahali kuweza kutia sahihi sehemu yoyote.

Wiki hii hatahivyo ilianza Jumatatu 8, Septemba ikiangazia tamko la haki kwa watoto wasiosikia, Jumanne 9, kuleta ufahamu ulimwenguni , Jumatano 20, kutambua kauli ‘ hakuna lolote bila sisi’, Alhamisi 21, kuwaeka watu wasiosikia katika ajenda, Ijumaa 22, Kufikisha haki za lugha ya ishara kwa wote na Jumamosi 23, ikiangazia ujenzi wajamii ya pamoja kwa watu wasiosikia.

BY EDITORIAL DESK