HabariKimataifa

Wakuu wa Chama cha NUP Watiwa tumbo Joto, Uganda

Maafisa wakuu wa chama cha National Unity Platform (NUP) nchini Uganda wadaiwa kukamatwa na maafisa wa usalama.

Kulingana na kiongozi wa upinzani Robert Kyagulanyi almaarufu Bobi Wine, polisi walivamia makao makuu ya chama chao na kuwakamata katibu mkuu David Rubongoya na msemaji Joel Ssenyonyi ili kuwazuia kuhutubia nchi siku ya uhuru wa Uganda.

Viongozi hawa wakiwemo wafuasi wengine kadhaa wanazuiliwa katika Barabara ya Kira na vituo vingine vya polisi vinavyo zunguka jiji hilo takriban siku nne baada ya kyagulani kukamatwa  katika uwanja wa kimataifa wa Entebee muda mfupi baada ya kutua nchini kutoka safari ya Afrika Kusini na kusafirishwa hadi kusikojulikana kisha kuachiliwa baadae.

Swala hili lilipingwa na polisi waliodai kumsindikiza tu kutoka Uwanja wa Ndege hadi nyumbani kwake Magere na kutaja kukamatwa kwake kama uvumi

Kukamatwa kwao kumejiri wakati Rais Yoweri Museveni akiongoza sherehe za kitaifa za Siku ya Uhuru katika viwanja vya Kololo.

BY EDITORIAL DESK