HabariNews

‘Mombasa Yangu’ yaboresha Usalama Mombasa Asema Gavana Nassir

Viwango vya utovu wa usalama vimepungua Mombasa ikilinganishwa na hapo awali. Hii ni kulingana na kauli ya Gavana wa Mombasa Abdul Swamad Sharrif Nassir.

Kwa mujibu wa Nassir, mpango wa ‘Mombasa Yangu’ umeimarisha vijana wengi waliokuwa mtaani bila kazi hali aliyoitaja kuimarisha viwango vya usalama eneo hilo. Nassir alidokeza kuwa kwa kipindi cha miezi mitatu ijayo atazindua mradi wa kuwawezesha vijana .

Sidhani kama crime levels ziko juu kama zilivyokuwa pale mwanzo, natamani kuweza kuwaajiri watu wote lakini ikiwa sheria imekufunga hakuna kitu naweza kufanya.Tukafanya mradi ule wa ‘Mombasa Yangu’, na sasa nimeweza kusema kitu kingine kuna mradi wa kuweza kuwawezesha hawa vijana wale amao wameonyesha wazi ya kua wako tayari kufanya kazi,” Alisema Nassir.

Kulingana na gavana Nassir mpango wa kuhamasisha wanafunzi wakati wa likizo(mentorship Programme) uliwezesha kwa hali ya juu kuwaepusha vijana wengi hasa wanafunzi  kutojihusisha na maswala ya utovu wa usalama.

Hali kadhalika Alidokeza kuwa baada ya mpango huo vijana hao wataweza kupelekwa katika vituo mbali mbali ili wapate fursa ya kujihusisha na maswala ya kijamii.

Tunahukua vijana siku ya likizo, kwanza katika ile motivation Yule kijana anaelezewa, anazungumziwa jinsi ya kutoingia katika mabaya, pili tunamtoa huyu kijana barazani kwa sababu wanaharibika wakiwa pale, na sasa hivi hii program kila ikiendelea wataanza kuchukuliwa wale vijana tuwapeleke katika hospitali zetu, nyumba za wazee , tuwapeleke katika orphanages waweze kuona umuhimu wake

BY MEDZA MDOE