HabariNews

Umasikini na Njaa Watajwa Kuchangia Uskwota Kilifi

Umaskini umetajwa kuwa donda sugu kwa wakaazi wengi  kaunti ya Kilifi hali inayowapelekea wenyeji kuuza mashamba yao kwa bei ya rejareja huku wakisalia masikwota.

Akizungumza katika mahojiano na Sauti ya Pwani, Mchanganuzi wa siasa Priscillah Munga alibainisha kuwa wakaazi wengi wamekuwa wakiuza mashamba yao kwa mabwenyenye na kusalia ombaomba kila kukicha.

Munga alitaja ukosefu wa hatimiliki za ardhi kuwa tatizo sugu kwa wakaazi wengi hali inayowasababishia kupokonywa ardhi zao na mabwenyenye huku akitoawito kwa wakaazi kukoma kuuza mashamba kwa bei ya kutupa badala yake kutafuta mbinu mbadala ya kujipatia riziki.

Ardhi nyingi zimmekuwa hazina title, unyakuzi umezidi sana yote yanaletwa na njaa pia.ukweli ni kwamba serikali ingeweza kuangazia sehemu zile zote ambazo hazina title ili wakaweza kusaidia watu, kuelimishwa pia ni vizuri. Waitwe nyanjani waweze kuelimishwa na waweze kujua ardhi umuhimu wake ni nini” Alisema

Vilevile vijana waliangukiwa na lawama za kiongozi huyu kwa kukosa kutilia manaani elimu hali inayowapelekea kukosa nafasi za kazi serikalini kutokana na ukosefu wa vyeti muhimu vya elimu na kuwataka kusitisha lawama kwa kukosa nafasi zinazowanufaisha wageni.

“Ingekuwa elimu inapewa kipao mbele, unaweza kuta kwamba kuna matangazo yamefanywa mtu hatalichukulia hilo jambo maanani ata hataki kusoma haya matangazo yanasema nini, baadaye watakuja kulaumu watakuta kwamba watu wanatolewa kutoka sehemu zingine waje wafanye hizo kazi.” Alisisitiza Munga

Munga aliyanena haya baada ya waziri wa elimu Ezekiel Machogue kuahidi kutoa chakula cha msaada hasa kwa shule zilizoko maeneo kame msimu huu wa mtihani unapokaribia ili kuwezesha wanafunzi kusalia shuleni.

 

BY EDITORIAL DESK