HabariNews

Sabina Chege asalim amri! Abanduliwa nafasi ya Kinara wa Wachache Bungeni

Hatimaye bunge limepitisha kubanduliwa kwa Naibu Kinara wa Wachache katika bunge la Kitaifa Sabina Chege.

Spika wa bunge la kitaifa Moses Wetangula amesitisha mvutano wa uongozi ulioibuka awali kwenye mrengo wa Azimio kufuatia suala hilo.

Mvutano huo ulianza mnamo Aprili 6 mwaka huu ambapo wabunge wa mrengo Azimio waliwasilisha ombi la kumbandua Chege ambaye ni mbunge maalum mamlakani na kupendekeza Mbunge wa Embakasi Magharibi Mark Mwenje kuchukua nafasi hiyo.

Hatua hii inajiri baada ya Mahakama kuu ya Kiambu kutupilia mbali kesi iliyowasilishwa na Chege kupinga kubanduliwa kwake na kumtaka kutumia chama chake kutatua mgogoro huo.

Kupitia hatua hiyo Mbunge wa Embakasi Magharibi Mark Mwenje sasa atahudumu kama Naibu Kinara wa Wachache katika mbunge la kitaifa akimsaidia kinara wake Mbunge wa Suna Mashariki, Junet Mohammed.

By News Desk