HabariMombasaNews

Wakazi Kukata KIU Mombasa! Serikali ya kaunti ikitia saini mkataba wa miaka 4 na Fresh Life

Tatizo la uhaba wa maji kwa wakazi wa kaunti ya Mombasa huenda likazikwa katika kaburi la sahau baada ya Serikali ya kaunti hiyo kutia saini mkataba wa miaka minne na kampuni ya kusafisha maji Fresh Life.

Kampuni hiyo ya usafishaji maji na masuala ya usafi ya ilitajwa kutoa suluhu kwa tatizo la uhaba wa maji na usafi wa mji.

Akihutubia wanahabari mkurugenzi mkuu wa Mombasa Coast Waters Abdulrahim Mohammed alisema mkataba huo unalenga kuongeza uzalishaji wa viwango vya maji na usafi mjini humo.

Aliongeza kuwa mkataba huo utasaidia kwenye tafiti za kutambua matatizo ya maji na usafi na pia kupata njia bora ya kutatua tatizo la maji Mombasa ili kuboresha maisha ya wakaazi.

tunapaswa kuwa na malengo yakuhakikisha kwamba watu wetu wanakuwa na maisha mazuri kama ilivyo sera ya gavana ambapo tunapaswa kuongeza upatikanaji wa maji na  usafi. “ Alisema

Kwa upande mkurugenzi mkuu mtendaji wa kampuni ya FRESH LIFE, Antony Mulinge alidokeza kuwa kupitia kwa ushirikiano wao na MAWASCO pamoja na serikali ya kaunti hiyo kutabuniwa nafasi za ajira kwa vijana wa maeneo ambayo yatachaguliwa kwenye mradi wa usafishaji ili kukinga jamii kutokana na magonjwa yanayosababishwa na uchafuzi wa mazingira kama vile cholera na kuendesha.

Tunatarajia kushirikiana na kaunti na mawasco kupunguza magonjwa yanayosababishwa na uchafu kama vile cholera na pia kutengeneza nafasi za ajira kwa vijana wa maeneo yatakayochaguliwa kunufaika na mradi huo.”Alisema Mulinge

Itakumbukwa kuwa suala la maji na usafi limekuwa kero kwa muda mrefu licha ya kaunti ya Mombasa kujitahidi kutafuta washirika na wawekezaji zaidi katika kukabiliana na suala hivi.

Awali Gavana wa Mombasa Abdulswamad Shariff Nasser baada ya kushirikiana na kampuni kadhaa alikariri kuwa Mahitaji ya maji Mombasa ni takribani cubic mita laki 2 huku maji yanayoingia Mombasa kwa siku moja yakiwa ni cubic mita elfu 50.

BY MJOMBA RASHID