HabariMombasaNews

Ndoto za Kuimarisha Uchumi Zafufuka, Meli ya Jolly Argento ikitia Nanga Bandarini

Shughuli za biashara na uchumi Bandarini Mombasa zinatarajiwa kuimarika zaidi kufuatia ujio wa Meli Kubwa iliyotia nanga bandarini humo.

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Meli ya Messina ukanda wa Afrika Mashariki na ambaye pia ni nahodha GiuseppeFedele, alidokeza kuwepo kwa mikakati ya kujenga kituo maalumu kitakachotumika kutua kwa meli ndani ya bandari ya Mombasa ili kurahisisha shughuli za usafirishaji wa makasha kwenye ukanda wa Afrika Mashariki.

Kwa upande wake Fedele, ipo haja ya kampuni hiyo kuwekeza zaidi katika kuleta meli kubwa humu nchini ili kuimarisha biashara suala analolitaja kuwa lenye uwezo wa kuongeza kipato cha bandari na kuenua uchumi wa taifa kwa jumla.

“Tumeamua kuekeza nchini Kenya sababu Kenya ni nchi nzuri ya kibiashara, hivyo tunatazamia kuekeza zaidi kutoka Mombasa mpaka Dar es salaam huku tukitumia Mombasa kama kitovu cha biashara zetu.Tuko na hata ndege ziko hapa nchini Kenya ambapo itasaidia kupanua zaidi katika sekta ya biashara huku tukitazama kuekeza kikamilifu katika mambo ya biashara zaidi.”Alisema Fedele

Nahodha Abdulaziz Mzee kutoka mamlaka ya usimamizi wa bandari nchini KPA alipongeza kampuni hiyo kwa kupiga hatua kutoka meli ndogo za hapo awali hadi kuleta meli kubwa. Suala hili Fidel alilitaja kuwa muhimu katika ustawishaji wa shughuli katika bandari ya Mombasa.

“Kulingana na Messina Line kwa mara ya kwanza kabisa wameleta meli kubwa katika Bandari yetu sababu kwa miaka mingi biashara zao zilikuwa za kuleta Roll on Roll Off na sasa kwa ujio wa meli hii tunatarajia biashara ziinuke zaidi katika nbandari yetu ya Mombasa”.Alisisitiza Nahonda Abdulaziz.

Haya yanajiri baada ya meli kubwa Jolly Argento ya kampuni ya meli ya Messina kutoka nchini Italy kutia nanga katika bandari ya Mombasa kwa mara ya kwanza siku ya Jumatano November 08, baada ya miaka mingi ya kuleta meli ndogo ndogo.

BY BEBI SHEMAWIA