HabariNews

Viongozi wa Dini waisihi Serikali kulitilia Maanani swala la Ongezeko la Utumizi wa Dawa za Kulevya Pwani

Utumizi wa dawa za kulevya ukitajwa kuwa tatizo kubwa na lililokita mizizi Pwani, viongozi wa dini wanaitaka serikali kutilia maanani swala hilo kwa kuimarisha vita dhidi ya dawa hizo ili kuokoa maisha ya vijana wengi wanaoangukia kwenye janga hilo.

Viongozi hao ukanda wa pwani wanaitaka serikali kukazia kamba vita dhidi ya utumizi wa dawa hizo ikizingatiwa kuwa tatizo hilo limechangia kuharibu maisha ya vijana wengi pamoja na kusababisha utovu wa usalama.

Wakiongozwa na askofu wa kanisa la kianglikana mjini Kilifi Reuben Shukuru Katite, walisema inasikitisha kuona kuwa ndoto za vijana zinaharibika kwa kiwango kikubwa huku wakimtaka naibu rais Rigathi Gachagua kuendeleza kampeni dhidi ya mihadarati hadi eneo la ukanda wa pwani.

NI jambo la kusikitisha na kuhuzunisha kwamba viana wetu wengi wamepotea katika madawa ya kulevya, nitoe wito kama kiongozi wa dini  kwamba serikali yetu ikaweze kuchukulia jambo hili na kulitilia manani na wakaweze kuja katika sehemu ya pwani na kuweza kusaidia vijana wetu. Naskuru muheshimiwa rais pamoja na naibu wake kwa kuweza kulichukulia jambo hili kwa uzito,” Alisema Katite

Katite alitoa wito kwa serikali kuhakikisha kuwa vituo vya matibabu ya waathiriwa wa utumizi wa dawa za kulevya vinajengwa kaunti ya Kilifi ili kuimarisha juhudi za kukabiliana na janga hilo.

Ni muhimu sana hasaa katika kaunti ya Kilifi ambapo tuna vijana wengi ambo wameathirika kuweze kuwa na kituo cha kuweza kusaidia vijana hawa. Niombe kwamba vituo hivyo vinaweza kufunguliwa kusaidia maana vijana niwengi , kwahivyo itakua bora kwa serikali kutilia maanani,” Aliongezea

Hayo yanajiri siku chache tu baada ya naibu rais Rigathi Gachagua kuahidi kuandaa kikao na wadau mbali mbali ili kupanga mikakati ya kukabiliana na swala zima la mihadarati katika ukanda wa pwani.

 

Hivi karibuni kabla hatujaenda krismasi, nitaweka kongamano na washikadau wote tuanze kuangalia hii mihadarati inayotuhangaisha hapa pwani tutafanya nini tukishirikiana na nyinyi, na tunataka kanisha na askofu mutusaidie muongee na watoto wetu na hata pia wale wanauza madawa ya kulevya kwa sababu wanatajirika wakiua na kuharibu watoto wa wenyewe,” Alisema Naibu rais Gachagua

BY ERIKSON KADZEHA