HabariMombasaNews

Mombasa yashirikiana na KeNHA Kukarabati Miundombinu na Kukabili Mafuriko;

Serikali ya kaunti ya Mombasa inalenga kushirikiana na halmashauri ya barabara nchini KeNHA ili kutatua tatizo sugu la mafuriko.

Akizungumza na wanahabari afisini mwake gavana wa Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir ametaja ushirikiano kama njia mwafaka ya kutatua tatizo hilo

Hii ni baada ya kushuhudiwa mafuriko ya mara kwa mara katika maeneo mbalimbali ya barabara mjini Mombasa.

Kulikuwa na tatizo kubwa sehemu ya Kibarani, tuliongea na KenHA tukawaonesha makosa yaliyofanyika walipokuwa wanatengeneza. Mara ya kwanza tukajaribu kurekebisha na sasa hivi wakakubali watafanya kazi na sisi.” alisema

Na upande wa Bombululu Barabara ile KeNHa wameweza kuandika barua na kutuma ile ilani, barabara ikijengwa iwe imepanda juu na kuna baadhi ya sehemu zingine kama serikali ya kaunti umechimba septic za kutosha lakini kutokana na hizi mvua zinajaa sana.

Tumeongea na Wahandisi na wakandarasi wa KenHa ile Barabara ikiwa inatengenezwa yale maji yote badala ya kuingia upande huu water flows with gravity wahakikishe yasiwe upande mmoja,” alisisitiza gavana Nassir.

Hata hivyo Nassir amesema serikali ya kaunti imepiga hatua kubwa katika kudhibiti mafuriko ukilinganisha na miaka ya nyuma.

“Upande wa Railway roundabout wakati nikichukua ofisi tuliona tatizo na leo hii kunanyesha but hata kama kuna maji na vile mvua ni nyingi there’s water but the water has moved, hata saa hii sehemu ya Bondeni, Marikiti maji yalikuwa yanakaa masaa kwa masaa na sasa hali ni tofauti, hata Coast general na Old town is not the way ilikuwa, Miritini Mwamlai kumebadilika tumerekebisha daraja huko,” alisema Nassir.

Haya yanajiri huku mafuriko yanayosababishwa na mvua inayoendelea kunyesha yakizidi kushudiwa katika maeneo mbalimbali nchini.

BY MJOMBA RASHID