HabariNews

Mtu mmoja Ajeruhiwa katika Mlipuko wa Meli ya Mafuta Mombasa

Mtu mmoja anaendelea kupokea matibabu katika hospitali moja kaunti ya mombasa baada ya mlipuko kutokea katika meli waliyokuwemo iliyoegesha katika bandari ya Mombasa eneo la Fisheries.

Kulingana na kaptain Vinit Kumar Shalmar ni kuwa wahandisi wa meli hiyo ya mafuta kwa jina EAST WIND II bado wanaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha mlipuko huo wakishirikia na maafisa wa polisi kutoka kituo cha ferry upande kisiwani.

Aidha Kumar ameeleza kuwa mwanamume mmoja kwa jina Rama Lugogo mwenye umri wa miaka 40 amekimbizwa hospitali ya Pandya akiwa na majeraha mabaya ambako anaendelea kupokea matibabu.

Hata hivyo, maafisa wa polisi na vitengo vya idara ya majanga na dharura wamefika sehemu hiyo kutathmini chanzo cha mlipuko huo.

BY SOPHIA ABDHI