Habari

Hospitali za Mshambani kutoza ada kwa wenye NHIF Wanaosaka Matibabu ya kutolazwa

Wakenya wanufaika wa Hazina ya Bima ya Kitaifa ya Afya NHIF maeneo ya mashambani sasa watakuwa wakilipia ada muhimu za matibabu.

Hatua hiyo inajiri baada ya Muungano wa Hospitali za Kibinafsi maeneo ya Mashambani nchin (Rural Private Hospital Association) RUPHA kuafikia uamuzi wao wa kusitisha utoaji wa baadhi ya huduma za matibabu kwa wagonjwa walio chini ya bima NHIF.

Muungano huo wiki jana ulikoa umetoa ilani ya kufanya hivyo kutokana na hatua ya Serikali kukawia kuusambaza wa fedha kwa muda wa miezi 6 sasa.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na Muungano huo umeafikia uamuzi huo kufuatia serikali kushindwa kufikia mwisho wa majadiliano ya kutafuta suluhu.

Kufuatia uamuzi hao miongoni mwa huduma zitakazoathirika zaidi ni huduma za wagonjwa wasiolazwa ambapo wenye NHIF watalazimika kulipia shilingi 1000 kwa matibabu.

Huduma nyinginezo muhimu zitakazolipiwa ni pamoja upasuaji ambapo wagonjwa watalipia ada za vyumba vya upasuaji na huduma za saratani ambapo walio na Bima ya NHIF watalipia ada ya ushauri wa utaalam wa daktari, vipimo vya maabara na ada nyinginezo za hatua za kimatibabu.

Kwa akina mama waja wazito walio na mpango wa Linda Mama pia watahitajika kulipa ada kwa kujifungua njia ya kawaida na huduma za kujifungua kupitia upasuaji.

Hata hivyo Kadhalika wahusika katika hospitali hizo wamesema kuwa wagonjwa wa dharura na wale waliopo katika hali maututi wataendelea kupata huduma hizo bila ya mabadiliko yoyote.

BY NEWS DESK