HabariNews

Mahakama ya upeo yakaa ombi la Jaji Chitembwe kuondoa mapendekezo ya kufutwa kwake

Mahakama ya upeo imetupilia mbali rufaa ya jaji wa zamani wa Mahakama Kuu Said Chitembwe ikisema kuna ushahidi wa kutosha unaoonyesha alihusika na ufisadi.

Jaji Chitembwe alikuwa amepinga pendekezo la kuondolewa kwake afisini baada ya aliyekuwa Gavana wa Nairobi Mike Sonko kutoa kanda za video na rekodi za simu za rununu zikimhusisha jaji huyo na ufisadi ila sasa juhudi za kulisafisha jina na kuokoa kazi yake zimegonga mwamba.

Awali jopo lililoteuliwa kumchunguza jaji huyo lilimpata na hatia ya kujadili namna ya kufanikisha kuondolewa kwa kesi katika Mahakama ya Rufaa huko Malindi kwenye makazi yake yaliyoko Mountain View eneo la Waiyaki Way Nairobi, mazungumzo aliyodaiwa kuyafanya na Jane Mutulu Kyengo, Mike Sonko, Jimmy Askar, Amana Saidi miongoni mwa wengine.

Mahakama hiyo imesisistiza kuwa ushahidi uliotolewa mbele ya jopo iliyoteuliwa kumchunguza ulithibitisha kuwa mwenendo wake ulikiuka Kanuni za Maadili ya Tume ya Huduma ya Mahakama na pia ulikuwa kinyume na ibara ya 168 kipengee cha 1(b) na kile cha (e) katika ibara hiyo yaa Katiba.

BY NEWS DESK