HabariNews

Familia ya Fatma Rajab Simenze yaomba msaada wako

Familia ya Rajab Simenze imewasilisha kilio cha msaada kwa serikali na wasamaria wema kote nchini ili kugharamia matibabau ya mpendwa wao Fatma Rajab Simenze.

Fatma mwenye umri wa miaka 26 alizaliwa na matatizo ya moyo aliyokuwa akiyamudu kutumia dawa ila hivi majuzi alikumbwa na changamoto za kiafya kufuatia suala hilo na kukimbizwa zahanati eneo la Kashani kisha kupelekwa katika hospitali kuu ukanda wa pwani maarufu COAST GENERAL anapoendelea kupokea matibabu.

 

Wazazi wa Fatma wameeleza changamoto inayokabili familia yao katika kugharamia matibabu ya mwanao.

Aidha wametoa wito kwa watu wote kujitokeza kuwasaidia kupata kiwango cha shilling millioni 1.8 ili kumwezesha mpendwa wao kufanyiwa upasuaji wa dharura wa moyo.

 

Ni huzuni kubwa kwa tasnia ya wanahabari  pamoja na  wafanyakazi wa Mo Radio anakofanyakazi kama mwandishi wa habari.

Dua zetu njema zi pamoja na familia hiyo na tunazidi kumwombea fatma shufaa ya haraka.

PAYBILL 200999

ACCOUNT NO 0771250013068

BY BEBI SHEMAWIA