HabariNews

Matokeo ya Mtihani KCSE 2023 Yatolewa, Watahiniwa 48,174 wakigonga Alama ya E

Watahaniwa 1,216 wamejizolea gredi ya A katika mtihani wa kitaifa wa KCSE mwaka wa 2023 hii ikiwa ni aslimia 0.14 ikilinganishwa na mwaka 2022 ambapo watanihiwa 1,146 walipata gredi ya A.

Watahaniniwa 201,133 wataweza kujiunga na vyuo vikuu baada ya kupata alama ya C+ huu na zaidi mwaka ikiwa ni asilimia 22.27 ikilinganishwa na 173,345 mwaka 2022 ikiwa ni asilimia 19.62.

Akizungumza wakati wa kutoa matokeo ya KCPE mwaka huu Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu amesema hatua hiyo ni kutoka na mfumo mpya wa utoaji alama kwa wanafunzi uliopunguza masomo yanayohitajika kutoa gredi ya wastani.

Watahiniwa 526,222 waliweza kupata alama ya D+ na zaidi mwaka 2023 hii ikiwa ni asilimia 58.27 ikilinganishwa mwaka wa 2022 ambapo wataniniwa 522,588 hii ikiwa ni asilimia 59.14.

Shule za kitaifa zilitoa watahiniwa 889 wenye alama ya A ikiwa ni asilimia 24.86 ikifuatwa na shule za kaunti ambazo zilitoa watahiniwa 172 wenye gredi ya A ikiwa ni asilimia 0.096 na za kibinafsi 143 ikiwa ni asilimia 0.221 na za kata dogo zititoa wanafunzi 7 wenye gredi ya A ikiwa ni asilimia 0.001.

Hata hivyo, watahiniwa 48,174 waliopata alama ya E, idadi hii kubwa kurekodiwa mwakahuu ilimpelekeanwaziri Machogu kuitisha uchunguzi wa mara moja ili kubaini kiini chake.

Naagiza kurugenzi ya uhakiki wa ubora kushirikiana na maafisa wa nyanjani pamoja na walimu kuchunguza kesi hizi za alama ya E katika kila kata nchini na kuwasilisha ripoti kwangu ndani ya mwezi mmoja kwa hatua zaidi,” alisema Machogu

BY NEWS DESK