HabariNews

Washukiwa wa ulangunzi wa pembe za Sh. 11.2M Washtakiwa Kwale

Washukiwa wawili wa ulanguzi wa Pembe za Ndovu wamefikishwa katika Mahakama ya Msambweni Kaunti ya Kwale na kushtakiwa na kosa la kupatikana na pembe hizo.

Wawili hao Tima Omar Suya na Bahatisha Juma Saidi walifikishwa mbele ya Hakimu Sandra Ogoch na kushtakiwa kwa kupatikana na pembe tano za ndovu zenye thamani ya shiligi Milioni 11.2.

Mashtaka dhidi yao ni kwamba mnamo tarehe 6 Mwezi Januari Mwaka huu katika eneo la Majoreni, Lunga Lunga walipatikana na pembe hizo zenye uzani wa kilo 111.98 zikiwa zimefichwa kwenye gunia na kusafirishwa katika gari moja bila kibali.

Tima pamoja na Batisha hata hivyo walikana mashtaka hayo na kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni 3 kila mmoja na mdhamini kiasi sawa na hicho.

Kesi hiyo itatajwa tena mnamo tarhe 24 Mwezi Januari na kuanza kusikilizwa tarehe 21 Mwezi Februari mwaka 2024.

BY NEWS DESK