HabariMombasaNewsSiasa

MKE WA MBUNGE WA CHANGAMWE OMAR MWINYI AAGA DUNIA.

Mkewe Mbunge wa Changamwe Omar Mwinyi ameaga dunia, baada ya kuugua ghafla.

Inaarifiwa kuwa Rukiya Khatibu Ali aliuugua ghafla Jumatatu usiku kabla kukimbizwa katika hospitali ya Pandya ambako alizidiwa alipokuwa akipokea matibabu.

Mwili wake tayari umerudishwa nyumbani kwake eneo la Potreitz Changamwe ambapo familia inaendelea na matayarisho ya mazishi.

Kulingana na msaidizi binafsi mbunge wa Changamwe Ibrahim Chilai mwendazake atazikwa leo eneo la Mwigo mwendo was aa saba baada ya swala ya Adhuhuri.

Viongozi mbali mbali wanaendelea kutuma risala zao za rambi rambi kwa familia ya mbunge huyo kufuatia kifo cha mkewe wakimtaja mwendazake Bi. Rukiya kama mama aliyekuwa na msimamo na mapenzi kwa jamii

Chama cha ODM mapema leo kimetuma ujumbe wake wa rambi rambi kwa mbunge Omar Mwinyi kikimuombea kwa Mungu kumpa uvumilivu na utulivu kutokana na msiba huo.

BY EDITORIAL DESK