HabariNewsWorld

Mahakama DRC Kuamua Kesi ya Kupinga Matokeo ya Uchaguzi

Mahakama ya kikatiba nchini DRC, inatarajiwa kutoa uamuzi wake kuhusu kesi ya kupinga matekeo ya uchaguzi wa urais, tarehe 12 mwezi huu.

Ni Kesi iliyokuwa imewasilishwa mahakamani na mmoja wa wagombea Theodore Ngoy Ilunga, akitaka matokeo ya uchaguzi wa urais wa Disemba 20, kufutiliwa mbali kwa msingi kwamba uchaguzi huo ulikumbwa na matatizo mengi ya kiufundi na udanganyifu.

Sasa Mahakama hiyo inatarajiwa kutoa uamuzi huo Janauri 12, baada ya kuskiza kesi hiyo Jumatatu, ambapo upande wa rais Felix Tshisekedi aliyetengazwa mshindi wa uchaguzi huo kujitetea mahakama pamoja na tume ya uchaguzi, CENI.

Licha ya kuonesha kutoridhishwa na matekeo ya uchaguzi wa urais, upande wa Wapinzani wakuu ambao ni Moïse Katumbi na Martin Fayulu haukufika mahakamani kupinga matokeo hayo, wakidai mahakama ya kikatiba inaegemea upande wa serikali.

BY NEWS DESK