HabariNews

Tamu na Chungu ya Elimu Yawakabili Wazazi

Zaidi ya wanafunzi milioni 1.4 waliofanya Mtihani wa Kitaifa wa KCPE mwaka 2023 wanaendelea kusajiliwa katika shule mbali mbali humu Nchini.

Wanafunzi hao wanajiunga na shule hizo wakati ambapo Wabunge wanaendelea kulalamikia kucheleweshwa kwa usambazaji wa fedha za ustawishaji maeneo Bunge NG- CDF, fedha ambazo zinategemewa pakubwa na wanafunzi kutoka kwa familia zisizojiweza.

Baadhi ya wabunge ukanda wa Pwani wakiongozwa na mbunge wa Malindi Amina Mnyazi walishinikiza serikali kusambaza fedha za hazina ya CDF kwa maeneo bunge ili kuwasaidia wanafunzi kwa kwaro.

Wazazi aidha walilalamikia kuhusu ongezeko la karo katika baadhi ya shule licha ya Serikali kutoa mwongozo wa karo.

Wanafunzi hao wanajiunga na Shule za Sekondari wakati Wakenya wanaendelea kulalamikia gharama ya maisha huku wazazi wengi wakihofia kwamba huenda watoto wao hawataripoti shuleni kufuatia ukosefu wa karo.

Baadhi ya walimu wakuu wa shule za upili eneo bunge la Voi kaunti ya Taita Taveta walieleza kuweka mikakati mwafaka kuhakikisha wanafunzi wanajiunga na shule za upili ikiwemo hata kulipa karo nusu au kwa awamu.

Walitoa wito hata hivyo kwa wazazi kuhakikisha wanafunzi wanajiunga na kidato cha kwanza haraka ili masomo yaanze kwa wakati kama yalivyoratibiwa.

“ Tunaandikishana mkataba na wao ili tuhakikishe ya kwamba mtoto amebaki shuleni aendelee na masomo na mzazi nae aendelee kutafuta ili awezekukamilisha karo yake.

Tumekuta kuwa wazazi wengi kupata fedha imekua ni ngumu, wengine wanakuja na karo nusu, lakini kama shule tumekaa na walimu wakuu wa shule nyingi na tumesema wazazi tuwasaidie

 

NA HUKO, Kaunti ya Kwale zaidi ya wanafunzi 900 wanaojiunga na Shule za Upili za Kitaifa wamepata ufadhili wa masomo wa takriban kima cha shilingi Milioni 35 kwa hisani ya Serikali ya Kaunti hiyo.

Akizungumza wakati wa kutoa ufadhili huo, Gavana wa Kaunti hiyo Fatuma Achani, aliwahimiza wanafunzi hao kutia bidii katika masomo yao kwani ndio msingi wa maisha yao.

Niwapongeze wale watot wetu wote ambao walifanya vizzuri na wanaenda kujiunga na shule za sekondari, nyinyi ni kama mabalozi wetu hii pesa ambayo tunaenda kupeana 35M ni pesa nyingi sana sisi tunaomba tu wewe usome utuletee matokeo mazuri” Alisema Achani

Kwa upande wake Mbunge wa Matuga Kassim Sawa Tandaza alisema kuna haja viongozi wa eneo hilo kushirikiana kuipa nguvu elimu ili kuhakikisha wanafunzi wanafanya vyema.

Tandaza aidha alitoa wito kwa wanafunzi waliomaliza kidato cha 4 na ambao hawakupata alama za kujiunga na vyuo vikuu kuhakikisha wanajiunga na vyuo vya kiufundi ili kuijiimarisha na kuendeleza jamii.

Karibuni tunafungua ile chuo cha kiufundi pale Kwale, ni kituo cha kiserikali ambacho kitatoa certificate na diploma kwa upande wa ufundi, wazazi wajitayarishe kuleta watoto wao pale wwale ambao hatatakuwa wamejiunga na vyuo vikuu” Alisisitiza Tandaza

BY NEWS DESK