HabariNews

Mahakama ya Mtandao Kurahisisha Mchakato wa Haki

Jamii inahimizwa kutumia mfumo wamahakama za kushughulikia mizozo midogo ili kuharakisha mchakato wa kuapata haki.

Akizungumza na wahahari pambizoni mwa warsha ya kuhamasisha wadau kuhusu huduma za haki kupitia mtandao Mkurugenzi mkuu wa shirika la kuteta haki za kibinadamu Naila Abdallah alisema mfumo huo utasaidia pakubwa wananchi wenye uwezo mdogo kupata haki yao kwa wakati.

Naila ambaye pia ni mwanaharakati wa kutetea haki na maswala ya watoto vijana na kina mama kutoka shirika la Sisters for Justice alisema mfumo huu unamwezesha mtu kufangua mashataka akiwa mtandaoni bila kufika mahakamani.

Mtu anayedaiwa chini ya milioni 1 anaweza kufungu mashtaka kwa shilingi 1,000 zaidi katika masoko watu wanaweza kupeana na kuchukua mkopo lakini inapofika wakati wa wao kulipana kunakuwa na shida,pia kina mama wa vyama inafika mahali wanafika kulipa na mtu anachukuliwa vitu vya dhamana ya juu kuliko ile pesa aliweza kuchukua.” Alisema Naila.

Kwa upande wake Judy Philip ambaye ni mwanasheria kutoka mahakama kuu alisema kubuniwa kwa mahakama za kushughulikia madai na mizozo midogo midogo imelenga kumpunguzia mwananchi wa kawaida mahangaiko na gharama ya kusafiri kulipia mawakili mahakamani sawia na kupunguza mrundiko wa kesi mahakamani.

mahakama za kushughulikia mizozo midogo inafanya kazi kwa kuchukua kesi za thamani ya chini ya milioni 1,zile pesa ambazo unatumia kufungua mashataka kotini ni chini ya elfu moja kumanisha hutatumia pesa nyingi kufungua mashataka na pia maagizo ya kufuata ni rahisi kusaidia mtu popote alipo na inapeana hukumu chini ya siku 60.” Alisema Judy.

Naye Stephen Oguna kutoka shirika la kutoa hamasa kuhusu maswala ya kibinadamula Chema Initiative alidokeza kuwa wadai wengei wameshindwa kwenda kotini akisema mfumo huo umerahisisha mambo hata zaidi.

Kesi zimekuwa nyingi ukiangalia kipengele cha 159 2c ya katiba yetu kinapatia uhuru wa kuzingatia njia zingine za kusuluhisha migogoro katika jamii na mahakama za kushughulikia mizozo midogo ni mojayao na leo tunapigia mpato kwa sababu mtu wa pale chini hawezi kulipa fidia ya wakili.” Alisema Oguna

By Medza Mdoe