HabariNews

Pigo kwa Chama cha PAA, ODM Ikivuna Wanachama wake Wapya

Spika wa Bunge la Seneti Amason Kingi amepata pigo baada ya baadhi ya wakuu wa chama cha PAA kuhama na  kujiunga na chama cha ODM.

Katika hatua ambayo inaonekana kuchukua mkondo tata kwenye siasa za kaunti ya Kilifi na Pwani kwa jumla,viongozi hao walilalamikia kutelekezwa na mkuu wa chama hicho Amason Kingi.

walidai kuwa Kingi ametekeleza maslahi yake binafsi na kuwaacha mataani kufuatia makubaliano yake na serikali ya kenya kwanza wakisema kuwa hawakuwa wakihusishwa katika maamuzi muhimu ya chama hicho.

Waasi hao walikutana na kinara wa Azimio Raila Odinga katika jengo la Chungwa kufanikisha mchakato wa kujiunga rasmi na chama hicho.

Akizungumza baada ya kukutana na kuwakaribisha wanachama hao Odinga alisisitiza kuwa wanachama wa Azimio waliohamia Kenya Kwanza hawapaswi kurejea chamani bali wajiuzulu ili kupisha uchaguzi mwingine.

Hawa ni watu ambao hata hawana viti vyovyote lakini wameamua kisera wanataka kurudi kuungana na ODM, hii ni tofauti na wale wabunge ambao wanaruka , wanaangalia katika nyumba ile nyingine , wale ndio tumesema warudi kwa wananchi wachaguliwe upya tena” Alisisitiza

Viongozi hao ni akiwemo kiongozi wa vijana wa chama cha PAA kaunti ya Kilifi Sammy Nyundo.

BY  NEWS DESK