HabariNews

Hatutingishiki Kamwe! Raila Odinga awahakikishia Wakenya

Kinara wa Azimio Raila Odinga amezuru kaunti ya Lamu hapa pwani kutathmini zoezi wa usajili wa wanachama wapya katika chama cha ODM.

Odinga aliandamana na viongozi mbali mbali wa chama hicho ikiwa ni katika harakati za kushawishi viongozi wa vyama vingine vya kisiasa kujiunga na chama hicho

Akizungumza eneo hilo Odinga alisema zoezi la usajili limekuwa likiendelea katika sehemu mbali mbali hapa nchini na wanatarajia kuona wanachama wapya wanajiunga na ODM ili kupata uungwaji mkono katika uchaguzi mkuu ujao.

Hakuna hatari kwamba Azimio itaanguka hivi karibuni, hakuna mtu aliyeondoka Azimio imesalia sawa isipokuwa wabunge wachache ambao wameamua kujiondoa,
Uongozi wa Azimio uko shwari, hakuna mafarakano popote pale Azimio ” Raila alisema

Aliyekuwa gavana wa Kakamega ambaye pia ni Naibu mwenyekiti wa kitaifa wa chama hicho Wyclife Opranya alitilia mkazo kuwa ziara hiyo inalenga kuhakikisha chama cha ODM kinapata nguvu hata ifikapo mwaka 2027 kinyakue serikali.

Tunataka chama chetu kiwe na nguvu, nataka niwahakikishie watu wa lamu kule tuko kwa ODM tuko katika mrengo wa azimio na lengo letu nikuona kwamba chama chetu kiko na nguvu ili iifika mwaka 2027 tuko tayari kuchukua serikali kutoka kwa bwana Ruto” Alisema

Itakumbukwa kuwa wiki baadhi ya wafuasi wa chama cha PAA kaunti ya Kilifi waliaasi chama hicho na kujiunga na chama cha ODM.

BY NEWS DESK